Deuteronomy 1:2-6

2 a(Ni mwendo wa siku kumi na moja kutoka Horebu kwa njia ya Mlima Seiri mpaka Kadesh-Barnea.)

3 bKatika mwaka wa arobaini, siku ya kwanza ya mwezi wa kumi na moja, Musa aliwatangazia Waisraeli yale yote Bwana aliyomwamuru kuwahusu. 4 cHii ilikuwa baada ya kumshinda Sihoni mfalme wa Waamori, ambaye alitawala Heshboni, na pia huko Edrei alikuwa amemshinda Ogu mfalme wa Bashani, ambaye alitawala huko Ashtarothi. 5 dHuko mashariki ya Yordani katika nchi ya Moabu, Musa alianza kuielezea sheria hii, akisema:

6 e Bwana Mwenyezi Mungu wetu alisema nasi huko Horebu, “Mmekaa vya kutosha katika mlima huu.
Copyright information for SwhKC